Baraza la Madiwani H...
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Musoma latoa pongezi kwa MUWASA.
26 Nov, 2026
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Musoma latoa pongezi kwa MUWASA.

Wajumbe wa Baraza la madiwani katika Manispaa ya Musoma leo tarehe 26 Novemba, 2026 wameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) kwa kuendelea kuboresha utoaji wa huduma ya maji katika mitaa iliyopo Manispaa ya Musoma.

Pongezi hizo zimetolewa na Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Musoma kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichoongozwa na Msitahiki Meya wa Manispaa ya Musoma, Mhe. Alex Nyabiti.

Mkurugenzi Mtendaji wa MUWASA Bi. Esther Gilyoma alihudhuria kikao hicho cha Baraza la Madiwani ambacho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma na kuwasilisha taarifa ya Utendaji wa Mamlaka kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027.
KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE

slot gacor