OFA YA KURUDISHA HUD...
OFA YA KURUDISHA HUDUMA YA MAJI BILA FAINI
09 Oct, 2025

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma (MUWASA) inapenda kuwafahamisha Wananchi na Wateja wake kuwa, katika kuadhimishi Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025, Mamlaka  imetoa ofa maalum ya kuondoa faini ya kurejeshewa huduma ya maji (reconnection fee) kwa wateja waliokatiwa maji.

MUWASA inatoa wito kwa Wateja wote ambao huduma yao ya maji ilisitishwa kutokana na madeni ya bili za maji, wafike katika ofisi za MUWASA ili kuingia makubaliano ya kulipa madeni yao na kurejeshewa huduma ya maji bila kulipa faini

Usikose fursa hii muhimu! Ofa hii maalum inaanza tarehe 07.10.2025 hadi 30.10.2025.