TAARIFA YA UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI MUSOMA
03 Oct, 2025
Taarifa kwa Umma:
YAH: UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) inawatangazia Wateja wake na Wananchi kwa ujumla kuwa kuna ukosefu wa huduma ya Maji leo tarehe 03.10.2025 . kutokana na kupasuka kwa bomba kubwa eneo la Majengo.
Maeneo yatakayoathirika ni mtaa wa Majengo na baadhi ya eneo la Songe
Huduma itarejea mara baada ya matengenezo kukamilika
MUWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Tangazo hili limetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma leo tarehe 03.10.2025