TAARIFA YA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI MUSOMA
YAH: UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) inawatangazia Wateja wake na Wananchi kwa ujumla kuwa kutakuwa na upungufu wa huduma ya Maji na kwa baadhi ya maeneo na maeneo mengine kukosa kabisa huduma siku ya kesho tarehe 29.03.2026 kwa sababu ya kukatika kwa nishati ya umeme kwenye chanzo cha maji Bukanga.(kulingana na tangazo la Tanesco)
Maeneo yatakayoathirika ni mitaa yote ya Manispaa ya Musoma, pamoja na eneo la Nyabange, Etaro, Kurumuli na Mmahare.
MUWASA inawaomba Wateja wake kuchota maji na kuyahifadhi ili kuepuka adha ya kukosa maji.
MUWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Maeneo ya pembezoni huduma itachelewa kufika (Rwamlimi, Songambele, Nyabisare, Bweri-Bukoba, Buhare, Kwangwa na Nyabange)
Tangazo hili limetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma leo tarehe 28.03.2026

