TAARIFA YA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI MUSOMA
10 Aug, 2026
Taarifa kwa Umma:
YAH: UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) inawatangazia Wateja wake kuwa kutakuwa na upungufu wa huduma ya Maji kuanzia leo tarehe 09.08.2026 kutokana na kutokea kwa hitilafu kwenye mitambo ya kusukuma maji iliyopo Bukanga.
Maeneo yatakayoathirika ni baadhi ya Mitaa ya Manispaa ya Musoma hasa ya pembezoni na eneo la Nyabange
Huduma itaimarika mara baada ya marekebisho ya hitilafu kukamilika.
MUWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Taarifa hii imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma leo tarehe 10.08.2026

