Mwenge wa Uhuru 2026 waweka Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Mita za Malipo ya Kabla
MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI LA UZINDUZI WA MITA ZA MALIPO YA KABLA (PRE-PAID WATER METERS) KATIKA MANISPAA YA MUSOMA
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 ndugu Wazo Michael Mwang'onda ameweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ufungaji wa mita za malipo ya kabla leo tarehe 07 Agosti, 2026 ikiwa ni Utekelezaji wa agizo la Serikali kwa wananchi kuhakikisha wanajua matumizi sahihi ya maji na kuepuka bili kubwa zisizotarajiwa.
Ufungaji wa mita za malipo ya kabla unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) ambapo mita hizo za malipo ya kabla una gharama ya shilingi za Kitanzania milioni 177 ikiwa ni kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani ya Mamlaka.
MUWASA inaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 95 ndani ya Manispaa ya Musoma.
KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE

