Bodi ya Wakurugenzi...
Bodi ya Wakurugenzi MUWASA yafanya ziara ya kutembelea Mradi wa Majitaka na eneo la chanzo cha maji
14 Feb, 2026
Bodi ya Wakurugenzi MUWASA yafanya ziara ya kutembelea Mradi wa Majitaka na eneo la chanzo cha maji

BODI YA WAKURUGENZI MUWASA YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MRADI WA MAJITAKA NA ENEO LA CHANZO CHA MAJI

Bodi Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) imefanya ziara ya Kutembelea maneno yake ya miradi inayosimamiwa na MUWASA.

Bodi hiyo ya Wakurugenzi, inayoongozwa na Mwenyekiti Dkt. Felix Gadi Oning'o (KIVUYO)     
ilifanya ziara mara baada ya kumaliza  kikao cha Bodi cha Robo ya Pili kwa mwaka wa Fedha 2025/2026

Wakurugenzi wa Bodi waliambatana na wajumbe wa Menejimenti ya MUWASA ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi alitoa maagizo kwa Menejimenti ya MUWASA kuhakikisha kuwa Mradi wa Majitaka unatoa huduma ya Usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Musoma kwa ufanisi kwa sababu ni mradi Mpya wenye lengo la kuweka Mazingira safi na salama kwa wakaazi wa Manispaa ya Musoma.

Aidha, Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) imeipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutekeleza Mradi wa Majitaka Katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma wenye lengo la kuboresha Usafi wa Mazingira kwa wakaazi wa Manispaa ya Musoma.

Mradi huo wa Majitaka ambao umekamilika kwa awamu ya kwanza umeanza kutoa huduma kwa takribani wananchi 514 ambao wameungwa moja kwa moja kwenye mfumo wa uondoshaji wa majitaka kwenye makaazi yao.

Mradi huo ambao umegharimu jumla ya tsh. Bilioni 31unatarajia  kunufaisha wananchi waliopo katika  Kata za Iringo, Mukendo, Mwigobero na Kitaji

Wakurugenzi wa Bodi walionesha kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa majukumu na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya Majisafi na uondoshaji wa majitaka. 

Sambamba na hilo, Wakurugenzi wa Bodi ya MUWASA walitembelea chanzo cha maji kilichopo eneo la Bukanga na kujionea namna mbalimbali ya uzalishaji wa maji hadi kuwafikia wananchi. 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MUWASA Mhandisi Nicas Mugisha alitoa shukrani kwa Wakurugenzi wa Bodi kwa kuwahakikishia kuwa huduma zitolewazo na MUWASA ni endelevu na zinazingia weledi.