HALI YA UPATIKANAJI...
HALI YA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI KATIKA MAENEO YENYE UPUNGUFU.
18 Aug, 2026

TAARIFA KWA WAKAZI WA MUSOMA NA KIJIJI CHA NYABANGE

HALI YA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI KATIKA MAENEO YENYE UPUNGUFU.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) inawatangazia Wananchi na Wateja wake kuwa kumetokea changamoto katika mitambo ya uzalishaji Maji hivyo kupelekea MUWASA kutoa huduma ya maji kwa ratiba kwa baadhi ya  maeneo yote yaliyoathirika.

MUWASA inawaomba wateja wake kuzingatia ratiba ya upatikanaji wa huduma itakayotolewa sambamba na kuhifadhi Maji kwa wingi na kuyatumia kwa matumizi muhimu.

Ratiba ya upatikanaji wa Maji itafanyika kwa kipindi chote ambacho Mamlaka inafanya matengenezo ya mitambo na itapatikana katika kurasa za mitandao za Mamlaka na Ofisi za Watendaji wa Kata.

MUWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma 
18.08.2026

slot gacor